Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 04:41

Watu zaidi ya 60 wafariki katika ajali ya meli Comoro


Ramani ya visiwa vya Comoros
Ramani ya visiwa vya Comoros

Taarifa zinasema miili ya watu 50 imepatikana katika bahari iliyochafuka huku kundi la uokozi likiendelea kutafuta miili mingine iliyokwama

Takriban zaidi ya watu 60 wakiwemo watoto wanasadikiwa kuwa wamekufa baada ya meli ndogo ya abiria kuzama katika visiwa vya Comoro jumanne.

Maafisa wa Comoro wanasema idadi ya vifo inaweza kuongezeka katika ajali hiyo ya meli iliyokuwa na abiria 100. Haijafahamika haraka chanzo cha kuzama boti hiyo .

Tayari kundi la uokozi liko katika eneo la tukio katika bahari iliyochafuka.

Comoro inavisiwa vitatu kutoka ufukwe wa msumbiji. Meli hiyo ilikuwa inasafiri katika kisiwa kikubwa cha Grande Comore na kisiwa cha Anjouan.

Lakini shirika la habari ya kimataifa Reuters limemnukuu mwendesha mashtaka wa umma Soilih Mahmoud akisema kuwa meli hiyo ilikuwa inatokea mji mkuu wa Moroni kwenda kisiwa cha Anjoun na kugonga mawe takriban kilomita tatu nje ya ufukwe wa kisiwa kikubwa na kupelekea boti hiyo kuzama .

Shirika hilo linasema miili ya watu 60 imepatikana lakini mingine bado imekwama na itaweza kuondolewa pale bahari itakapotulia.

Baadhi ya watu walionusurika waliweza kuogelea mpaka eneo salama.
Nalo shirika la msalaba mwekundu linasema watu wengine walionusurika walipelekwa katika hospitali za Ouzioine na Foumbouni.

XS
SM
MD
LG