Licha ya mafanikio hayo, matumaini yanapotea kwamba kuna waathirika zaidi watapatikana wakiwa hai.
Katika mji wa kusini mwa Islahiye, katika jimbo la Gaziantep, waokoaji waliwamtoa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 40, wakati katika jimbo la kusini la Hatay, msichana mwenye umri wa miaka 13 aliokolewa baada ya kukaa kwa saa 182 chini ya kifusi ambapo tukio hilo liliwafanya waokoaji kushangilia.
Televisheni ya Uturuki ililionyesha eneo la tukio la watu wengine kadhaa wakiwa wanaokolewa Jumatatu, lakini wataalamu wameonya kwamba muda unazidi kwenda na kuwa vigumu kuwapata watu wakiwa hai katika majengo ambayo yameanguka.