Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 19:24

Watu wenye silaha wavamia hospitali mbili Nigeria


Wanaume watatu, katikati, waliotambuliwa kuwa watekaji nyara wa wanafunzi wa Shule ya Upili ya The Bethel Baptist wanaonyeshwa kwenye vyombo vya habari mjini Abuja, Nigeria, Alhamisi, Septemba 23, 2021.

Watu wenye silaha walivamia hospitali mbili katika mashambulizi tofauti kaskazini-magharibi na katikati mwa Nigeria, afisa wa eneo hilo na shirika la misaada walisema Jumanne.

Wahalifu wenye silaha nzito wanaojulikana na wenyeji kama majambazi wamesababisha uharibifu katika eneo hilo kwa miaka kadhaa licha ya majaribio ya makubaliano ya amani na kutumwa kwa askari.

Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) walisema watu wenye silaha walishambulia kituo cha afya katika kata ya Birnin Magaji katika wilaya ya Gummi katika jimbo la Zamfara siku ya Jumatatu, na kumteka nyara mtu mmoja.

Kundi lililojihami kwa silaha lilivamia kituo cha afya na kuwateka nyara mzee mmoja mfanyakazi wa uuguzi. MSF ilisema katika taarifa kwenye Twitter siku ya Jumanne.

Watu hao wenye silaha baadaye waliharibu dawa na chakula cha matibabu, iliongeza.

Shirika hilo la misaada linasaidia kuendesha sehemu ya kituo kinachosaidia watoto wenye utapiamlo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG