Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 09, 2025 Local time: 20:51

Watu wawili zaidi waathiriwa na sumu inayouwa nerve Uingereza


Maafisa wa polisi Uingereza wakilinda nje ya duka la madawa mjini Amesbury, Julai 4, 2018.
Maafisa wa polisi Uingereza wakilinda nje ya duka la madawa mjini Amesbury, Julai 4, 2018.

Polisi nchini Uingereza wanaopambana na ugaidi Alhamisi wanachunguza jinsi gani mwanamume na mwanamke waliathiriwa na sumu inayouwa nerve iliyotumika mapema mwaka 2018 dhidi ya jasusi wa zamani na mtoto wake wa kike.

Waziri wa Mambo ya Ndani Sajid Javid anaongoza mkutano wa kamati ya serikali inayoshughulika masuala ya dharura.

Watu hao wawili waliotambuliwa na marafiki zao kama Dawn Sturgess (44) na Charlie Rowley (45), walikutwa hawana fahamu Jumamosi huko mji wa Amesbury, kilomita 13 kutoka mji wa Salisbury, ambako Sergei Skripal na mtoto wake wa kike Yulla walikutwa na hali hiyo pia mwezi Machi.

Waziri wa Usalama Ben Wallace ameiambia BBC Alhamisi kuwa wachunguzi wana amini tukio jingine la sumu ni athari ya tukio la mwezi Machi na sio shambulizi jipya lililoelekezwa kwa Sturgess na Rowley.

Kitendo ambacho hakikutarajiwa cha kupewa sumu watu hao wawili, ambao hawana mafungamano yoyote na Russia, kimeleta wasiwasi mkubwa kwa umma katika eneo la Salisbury. Maafisa wa afya wanasema kiwango cha hatari hiyo kwa umma ni cha chini mno.

Uingereza imeilaumu Russia kwa kuwashambulia kwa sumu familia ya Skripals kwa aina ya gesi inayoitwa Novichok, iliyotengenezwa na Soviet Union wakati wa Vita Baridi.

Wallace ameitaka Russia kutoa taarifa juu ya sumu hiyo.

Russia imekanusha kuhusika kwa namna yoyote na shambulizi hilo na badala yake imedai kuwa Uingereza yenyewe ni ya kulaumiwa kwa shambulizi hilo, katika jaribio la kuendeleza chuki dhidi ya Russia.

Kremlin imesema Alhamisi ilikuwa iko tayari kuisaidia Uingereza katika uchunguzi wa shambulizi dhidi ya Skripal, lakini Uingereza imekataa.

Shambulizi hilo la sumu lilisababisha kufukuzwa kwa idadi kubwa kuliko yoyote nyingine ya wanadiplomasia tangu kuanza kwa Vita Baridi wakati Marekani na Washirika wake Uingereza, Umoja wa Ulaya wakiwa upande wa Uingereza katika kuilaumu Moscow.

XS
SM
MD
LG