Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 03:20

Watu watatu waokolewa wakiwa hai baada ya saa 32 Ecuador


Waokoaji nchini Ecuador walifanikiwa kuwaokoa watu 3 wakiwa hai baada ya kufunikwa katika kifusi kwa zaidi ya saa 32.

Watu hao waliokolewa katika sehemu ya manunuzi ambayo iliharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi la siku ya Jumapili.

Picha za televisheni za hatua za uokozi katika mji wa bandari wa Manta umewapa watu wa Ecuador ahueni kwamba watu ambao bado hawajapatikana wanaweza kuwa hai.

Licha ya watu hao kuokolewa idadi ya vifo vya tetemeko hili la kipimo cha rikta 7.8 mpaka Jumatatu usiku ilifikia 410.

Tetemeko hilo lililotokea pwani ya kaskazini magharibi inaelezwa kuwa tukio baya kuliko nchini Ecuador katika kipindi cha zaidi ya nusu karne.

Mpaka sasa watu 2,500 wamejeruhiwa na maelfu kuachwa wakiwa hawana makazi.

XS
SM
MD
LG