Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 31, 2023 Local time: 02:06

Watu watano wauwawa kwa bomu Mogadishu


Kundi la al-Shabab pia lilishambulia gari lililobeba wafanyakazi wa UNICEF huko Gorowe

Watu wasiopungua watano waliuwawa Jumanne wakati bomu moja lililotegwa kwenye gari lilipolipuka nje ya mgahawa mmoja wenye harakati nyingi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Mwandishi wa habari wa Sauti ya Amerika-VOA-akiwa kwenye eneo alisema wanawake wawili walikuwa miongoni mwa watu waliofariki kutokana na mlipuko huo.

Daktari Abdulkadir Abdirahman Aden aliiambia Idhaa ya Kisomali ya Sauti ya Amerika kwamba watu sita wengine walijeruhiwa katika mlipuko huo na alisema idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Mgahawa uliolengwa upo karibu na Central Hotel
Mgahawa uliolengwa upo karibu na Central Hotel

Mgahawa uliolengwa upo karibu na “Hotel Central” ambayo ni maarufu kwa wafanyakazi waliopo kwenye makazi ya Rais wa Somalia.

Hakukuwa na madai ya haraka ya uwajibikaji juu ya tukio hilo lakini dhana imewekwa kwa kundi la wanamgambo wa al-Shabab lenye makao yake nchini Somalia ambalo limekuwa likifanya mashambulizi ya kujitoa mhanga mara kwa mara katika mji huo.

Jumatatu kundi hilo la al-Shabab lilidai kuhusika kwa bomu la kujitoa mhanga ambalo liliuwa watu wasiopungua saba na kuwajeruhi wanane wengine kaskazini mwa Somalia. Mshambuliaji wa tukio la Jumatatu alilenga basi dogo lililowabeba wafanya kazi wa shirika la kuhudumia watoto katika Umoja wa Mataifa-UNICEF kwenye mji wa Gorowe wakati wafanyakazi hao wakisafiri kutoka kwenye nyumba zao za wageni walikofikia kuelekea kazini.

XS
SM
MD
LG