Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 21:33

Watu watano wauawa katika mlipuko wa bomu mjini Mogadishu


Ramani ya Somalia
Ramani ya Somalia

Watu watano waliuawa Jumapili jioni katika mlipuko mkubwa wa bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye mgahawa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, uliokuwa umejaa mashabiki wa soka wakitizama fainali ya Euro 2024, vyombo vya habari vya ndani vilisema, vikinuku polisi.

Picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha moto mkubwa na moshi mwingi ukifuka angani usiku, huku mlipuko huo ukitokea kwenye mgahawa huo maarufu mjini kati.

“Bomu lililotegwa ndani ya gari lilipuka usiku nje ya mgahawa wa Top Coffee Restaurant, limewekwa na magaidi wa Kharijite,” shirika la habari la kitaifa la Somalia liliripoti, likitumia neno linalotumiwa na maafisa kuelezea kundi la wanajihadi la Al-Shabab lenye uhusiano na Al Qaeda.

“Ripoti za awali za polisi zinathibitisha vifo vitano na watu 20 waliojeruhiwa,” shirika la habari la SONNA limemnuku msemaji wa polisi Meja Abdifitah Aden Hassan akikiambia chombo cha habari cha serikali.

Televisheni ya taifa ya Somalia iliripoti habari hiyo hiyo kuhusu shambulio hilo la bomu, ambalo lilifanyika wakati vijana walikuwa wakitizama mchezo kati ya Uhispania na Uingereza.

Mwandishi wa habari wa AFP alisema wazima moto, polisi na magari ya kubeba wagonjwa waliharakia kwenye eneo la mlipuko huo.

Polisi walizingira eneo hilo, ambalo liko karibu na kasri ya rais inayojulikana kama Villa Somalia na lilikuwa na shughuli nyingi wakati wa shambulio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG