Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 15:32

Watu sita wamefariki katika shambulizi la msikiti huko Canada.


Gari la wagonjwa limeegeshwa nje ya mskiti wa Quebec City uloshambuliwa Jumapili Jan. 29, 2017.
Gari la wagonjwa limeegeshwa nje ya mskiti wa Quebec City uloshambuliwa Jumapili Jan. 29, 2017.

Rais wa msikiti mkuu wa jiji la Quebec City nchini Canada anasema watu sita wameuwawa na wanane kujeruhiwa wakati wa shambulizi la risasi uliofanyika Jumapili jioni .

Shambulizi hilo lilitokea wakati darzeni ya watu walipokusanyika kwenye kituo cha kitamaduni cha kiislam cha Quebec kwa ajili ya sala ya jioni. Polisi walisema washukiwa wawili walikamatwa.

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau alisema kwenye mtandao wa twitter kwamba “leo usiku wa-Canada wanaomboleza watu waliouwawa katika shambulizi la kikatili kwenye msikiti mmoja huko Quebec City. Saala zangu ziwafikie waathirika na familia zao”.

Mwezi June mwaka 2016 kichwa cha nguruwe kiliachwa kwenye ngazi za mlango kwenye msikiti huo huo ambao umeshambuliwa Jumapili usiku.

XS
SM
MD
LG