Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:32

Watu wasiopungua 41 wafariki katika ajali Pakistan


Miili ya waathirika ikiwa kwenye mifuko huku watu wakifanya kazi katika eneo la ajali ya basi katika Wilaya ya Lasbela, mkoa wa Balochistan, Pakistan Januari 29, 2023.Reuters.

Takriban watu 41 walifariki dunia Jumapili kusini mwa Pakistan wakati basi lililokuwa likisafiri kutoka Quetta kwenda Karachi lilianguka kwenye Korongo katika wilaya ya Lasbela ya Balochistan.

Kamishna Msaidizi wa Lasbela Hamza Anjumk aliliambia gazeti la Dawn, la Pakistan, Kutokana na mwendo kasi, basi hilo liligonga nguzo ya daraja alipokuwa akigeuza kurudi upande mwingine karibu na Lasbela. Baadaye gari hilo lilizama kwenye korongo na kisha kuwaka moto.

Pia siku ya Jumapili, watoto 10 walifariki dunia wakati mashua yao ilipopinduka katika ziwa la Tanda Dam kaskazini magharibi mwa Pakistan, maafisa walisema.

Gazeti la The Dawn linaripoti kuwa watoto 17 na mwalimu mmoja waliokolewa na kwamba watoto wanne kati ya hao wako katika hali mbaya.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG