Shambulio hilo lililotokea saa mbili usiku Jumamosi, wakati wa harakati nyingi kwenye kituo hicho cha mabasi yanayoelekea magharibi mwa nchi. Polisi wanawanuku mashahidi wakisema wameona watu ndani ya gari lililokuwa linapita wakirusha karibu magruneti matatu.
Naibu msemaji wa polisi Charles Owino amewambia waandishi habari kwamba hilo ni shambulio lililofanywa na wafuasi wa Al-Shabab na kwamba wataendelea na vita, na watawakamata walohusika.
Majeshi ya Kenya kwa wakati huu yanaendelea na vita vya kuwasaka na kuwamaliza wapiganaji wa kundi hilo la wanaharakati wanaoshikilia sehemu kubwa ya Somalia ya kusini.
Hilo llikuwa shambulio la kwanza katika mji mkuu wa Nairobi tangu mashambulio mawili yaliyotokea mwezi Oktoba katika mji huo. Hata hivyo kumekuwepo na mlolongo wa mashambulio kama hayo huko kaskazini mashariki ya nchi, tangu wanajeshi wa Kenya kuivamia Somalia zaidi ya miezi mitano iliyopita.