Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:55

Watu wanaoishi karibu na uwanja wa ndege wa Nyerere wanataka kulipwa kabla upanuzi kufanyika


Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere

Raia wa Tanzania wanataka serikali kufanya upya tathimini ili kupisha upanuzi wa wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Takribani kaya 885,000 katika eneo la Kipunguni ‘A’ wanataka serikali ya Tanzania kufanya upya tathimini ya malipo katika maeneo yao ili kupisha mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Huku wakiitaka serikali hiyo kuleta watu wengine ambao watafanya tathimini na sio kurudiwa na walewale ambao wameonekana kukosa ushirikiano na wananchi hao.

Limekuwa ni jambo la kawaida pindi serikali inapo kuwa inatekeleza miradi yake kuwaacha wananchi na manung’uniko kwa walio wengi kutokana na kuto rizika na kile wanacho patiwa baada ya maeneo yao serikali kuyachukua hali inayo wafanya waendelee kuwa tegemezi na kurudi nyuma kiuchumi.

Mmoja wa wakazi wa Kipunguni ‘A’ jijini Dar es Salaam Sophia Waziri ambae eneo lake limechukuliwa kwa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias Nyerere amesema wakazi wengi hawajarizika na tathimini ambayo imefanyika hasa katika eneo la majengo ambapo tathimini hiyo hailingani na ujenzi wa nyakati hizi akiitaka serikali isimamie kupata haki yao.

‘‘Watu walewale walio fanya tathimini ndio hao hao wanawasomea ripoti zenu za mahesabu alafu hao hao tena wanarudi tena kwenye tathimini sio kwamba watafute timu nyengine ambao itakuja nawao kuakiki kuona sababu wakiwarudisha walewale bado kuna uwezekano wakuendelea kuumia’’ amesema Sophia Waziri

Aidha wakazi hao wanasema toka mwaka 1997 walisitisha kuendeleza maeneo yao kwa kuupisha mradi huo ambao uliwafanya kushidwa kujiendeleza kiuchumi hivyo ni wajibu wa serikali kufanya tathimini upya kwa sheria za sasa na kuondoa malalamiko yanayo endelea kwa wengi.

Raia wanataka ufafanuzi

Charles Wambura akizungumza na sauti ya Amerika amesema bado anahitaji ufafanuzi wa kina kwakuwa tathimini aliofanyiwa inampa maswali mengi na hailingani na thamani ya sasa katika upande wa nyumba na mazao licha ya eneo lake kuwa sehemu ya biashara.

‘Lakini ndugu mwandishi nashanga thamani yake nyumba ya vyumba vitano na mabanda matatu ni milioni ishirini na saba mia tano themanini na tisa elfu mia tisa na hamsini na moja eneo langu mimi ni town center kama tuko mjini kama ningeweza kumuuzia mwekezaji hapa akaweka perol station nazungumzia sehemu ya bilioni tatu mpaka mbili.’aliongezea Charles

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya viwanja vya ndenge Tanzania (TAA) Mussa Mbura amesema bado hawaja pokea malalamiko rasimi kutoka kwa wananchi kuwa hawakubaliani na uthamini ambao umefanyika nakuwataka wenye malalamiko wafike ofisini kwake.

‘Maafisa wangu wako pale kila siku kuanzia saa tatu mpaka saa kumi na moja jioni kama pana malalamiko maanaake wamewafikisha maafisa na yatakuja ofisini kwangu na ofisini kwangu kuko wazi muda wote na hatujapata malalamiko rasimi au vurugu.’amesema Mbura

Mussa Mbura ameongezea kusema kwa hatua ya sasa ya uthamini hawawezi kusema nilini wakazi wa eneo hilo wanapaswa kuondoka na kupisha upanuzi wa uwanja kwakuwa bado ni mapema sana.

Mwandishi: Amri Ramadhani, VOA, Dar es Salaam.

XS
SM
MD
LG