Waliojeruhiwa wako katika hali mbaya na wanapatiwa matibabu katika kituo cha afya cha eneo hilo, msimamizi wa eneo la Fizi katika jimbo la Kivu Kusini, Aime Kawaya Mutipula, alisema kwa njia ya simu.
Maporomoko ya ardhi ni ya kawaida katika vilima vyenye miteremko mashariki mwa Congo ambapo mvua kubwa inaweza kuenea na kuulainisha udongo. Lakini kuna uwezekano mkubwa wa kutokea ikiwa udongo umetibuliwa na shughuliza za uchimbaji madini, ukataji miti au ujenzi.
Mwezi Desemba, mvua kubwa iliyonyesha katika mji mkuu wa Congo Kinshasa ilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi ambayo yalisababisha vifo vya takriban watu 170.