Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 04:11

Watu wanane wafariki kwenye ajali ya treni ya India


Picha ya ajali ya treni ya India. Picha ya maktaba. Julai 7, 2023.
Picha ya ajali ya treni ya India. Picha ya maktaba. Julai 7, 2023.

Treni moja ya mizigo imegongana na nyingine ya abiria kwenye jimbo la mashariki mwa India la West Bengal mapema Jumatatu, na kuuwa takriban watu wanane, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Waziri Kiongozi wa jimbo hilo Mamata Banerjee, katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X amesema madaktari, timu za uokozi pamoja na magari ya kubeba wagonjwa, wako katika shughuli za uokoaji kwenye tukio la ajali, ambalo ni karibu na wilaya ya Darjeeling eneo la kitalii karibu na milima ya Himalaya.

Msemaji wa kampuni ya reli ya Northeast Frontier Sabyasachi De amesema kuwa watu watatu miongoni mwa wanane waliouwawa ni wafanyakazi wa reli.

Takriban wengine 25 wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo ambayo ilitokea karibu na kituo cha treni cha New Jalpaiguri.

Vituo vya televisheni vimeonyesha treni moja ikiigonga nyingine upande wa nyuma na kusababisha behewa lake moja kugeukia upande mwingine.

Mamlaka za reli zimeviambia vyombo vya habari kwamba ajali hiyo imesababishwa na treni ya mizigo ambayo haikusimama ilipohitajika. Mabehewa kadhaa ya kwenye treni ya abiria pia yanasemekana yaliondoka kwenye njia ya reli.

Forum

XS
SM
MD
LG