Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 03, 2022 Local time: 22:04

Watu waliokwama Wuhan waanza kurejea makwao


Watu wakiwa wamevalia maski wakiwasili katika stesheni ya treni ya Hankou huko Wuhan, China Aprili 08, 2020. Photo by Hector RETAMAL / AFP)

Maelfu kwa maelfu ya watu waliokuwa wamekwama katika mji wa Wuhan baada ya kutangazwa amri ya kuufunga mji huo kutokana na mlipuko wa COVID-19 wameonekana Jumatano wenye furaha wakati wakisubiri kuchukuwa usafiri wa umma.

Usafiri kuingia na kutoka katika mji huo uliokuwa kitovu cha mlipuko wa COVID-19, ulifunguliwa baada ya marufuku ya siku 76 kuondolewa Jumanne.

Maafisa wa mji huo wenye watu milioni 11, wanasema wanatarajia watu 55,000 waliokuwa wamekwama watasafiri kwa mabasi na treni hii leo.

Wengi wanarudi makwao baada ya muda huo wote wengi wakisema hawajawaona watoto au familia zao kwa karibu miezi miwili na nusu tangu kufungiwa hapo Januari 23.

Shirika la habari la China Xinhua linasema kutakuwa na karibu safari 200 za ndege kuingia na kutoka Wuhan Jumatano.

Watu walionekana kuwa wenye furaha nyingi walipokuwa wanasubiri kuondoka mjini Wuhan.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG