Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 08, 2024 Local time: 18:21

Somaliland yapokea wakimbizi kutoka Yemen


Mkimbizi wa Yemen akiwa Hargeisa, Somaliland akionyesha kitambulisho chake cha kitaifa kwenye kituo kinachohudumia raia wa Yemen.
Mkimbizi wa Yemen akiwa Hargeisa, Somaliland akionyesha kitambulisho chake cha kitaifa kwenye kituo kinachohudumia raia wa Yemen.

Katika hatua isiyo ya kawaida, watu kutoka taifa lililogubikwa na vita la Yemen wanakimbilia katika eneo ambalo raia wake wamesambaa dunia nzima kutokana na miongo kadhaa ya mapigano nchini mwao.

Katika mwaka uliopita nusu ya watu 176,000 ambao wamekimbia mzozo nchini Yemen wamekimbilia pembe ya Afrika kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi. Waafrika wengi wamerudi majumbani mwao lakini elfu 26 ni raia wa Yemen ambao hawana pa kwenda .

Wasiima Mohamed aliwasili Somaliland Februari na mke wake na watoto wawili wa kiume. Walikimbia Yemen baada ya wanamgambo wa Kihouthi kushambulia nyumba yao mjini Aden. Lakini kwa bahati nzuri familia yao haikuwepo nyumbani wakati huo lakini Mohamed aliamua kukimbilia Somaliland ambako alijuwa hakuna mapigano na moja ya sehemu chache itakayokubali kupokea hati ya kusafiria ya Yemen.

XS
SM
MD
LG