Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 00:54

Watu wa watatu wauwawa katika mapigano Tripoli


Picha ya maktaba

Takriban raia watatu wameuwawa usiku wa kuamkia Ijumaa katika mapigano baina ya wanamgambo mjini Tripoli, kwa mujibu wa tarifa ya idara ya huduma za dharura ya Ijumaa.

Mapambano yalianza Alhamisi usiku katika mji wa Ain Zara, kitongoji chenye wakazi wengi mashariki mwa Tripoli baina ya vikosi vya Al-Raada na vile vya kimapinduzi vya vya Tripoli, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari.

Yalikwenda mpaka saa za mapema Ijumaa kabla ya kusambaa katika maeneo mengine.

Raia watatu waliuwawa na wawili kujeruhiwa kwa mujibu wa Osama Ali kutoka idara ya huduma ya magari ya wagonjwa pale alipoongea na televisheni ya Al-Ahrar, na kuongeza kusema kwamba watu hao walipelekwa katika hospitali ya Tripoli.

Wanafunzi sita walikwamba kutokana na mapigano katika mabweni ya wanafunzi mpaka pale walipotolewa na idara ya huduma za dharura alisema Ali.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG