Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:32

Watu tisa wauwawa katika shambulizi Syria


Shambulizi la anga mapema Jumapili kwenye soko la mboga mboga lenye shughuli nyingi kaskazini magharibi mwa Syria limeua watu tisa, wanaharakati na maafisa wa huduma za kwanza kufika eneo hilo wamesema.

Wanaharakati na shirika la upinzani la waangalizi wa vita vya na haki za binadamu lenye makao yake Uingereza, Syrian Observatory limesema Russia, mshirika mkuu wa rais wa Syria, Bashar Assad, ilianzisha mashambulizi dhidi ya mji muhimu kijeshi, unaoshikiliwa na upinzani wa Jisr al-Shughur karibu na mpaka wa Uturuki.

Shambulio limetokea siku moja baada ya kundi la mamluki la Moscow kuasi kwa muda mfupi dhidi ya rais wa Russia, Vladimir Putin.

Shirika la ulinzi la raia linaloshikiliwa na upinzani kaskazini magharibi mwa Syria na kujulikana kama White Helmets limesema zaidi ya watu 30 walijeruhiwa, na wanatarajia idadi ya vifo kuongezeka.

“Tunasikia kwamba waliojeruhiwa vibaya wamekuwa wakifariki dunia baada ya kufika hospitali,” Ahmad Yaziji wa White Helmets ameiambia The Associated Press.

“Lilikuwa ni shambulio lililolengwa katika soko kuu la mboga mboga ambapo wakulima kutoka kaskazini mwa Syria hukusanyika.”

Forum

XS
SM
MD
LG