Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 07:04

Watu tisa wauawa kanisani Charleston, Marekani


Watu wakitafuta taarifa za ndugu zao baada ya shambulizi la kanisani huko Charleston, South Carolina, June 17, 2015.

Msako unaendelea huko kusini-mashariki mwa Marekani katika mji wa Charleston katika jimbo la South Carolina dhidi ya mtu mwenye silaha ambaye aliuwa watu tisa katika shambulizi la bunduki kwenye kanisa moja la kihistoria la wamarekani weusi jumatano usiku, shambulizi ambalo polisi wanalichunguza kama uhalifu wa chuki.

Picha na maelezo ya mshukiwa
Picha na maelezo ya mshukiwa

Mkuu wa polisi wa Charleston, Greg Mullen aliwaambia waandishi wa habari mapema alhamis kwamba mwanamme mmoja mzungu akiwa kwenye umri wa miaka ya 20 hivi aliingia kwenye kanisa la Emanuel African Methodist Episcopal wakati wa mkutano wa ibada ya wiki na alianza kufyatua risasi. Mullen alisema watu wanane walikufa kanisani humo huku mtu mwingine alikufa baada ya kupelekwa hospitali. Maafisa walitoa vipeperushi ambavyo vimeambatana na picha ya mshukiwa wakati akiingia ndani ya kanisa hilo.

Ripoti zinasema mchungaji wa kanisa, Clementa Pinckney, ambaye anahudumu katika baraza la wawakilishi la South Carolina kama seneta wa jimbo alikuwa miongoni mwa watu waliokufa katika shambulizi hilo. Watu kadhaa walijeruhiwa.

Polisi katika eneo la tukio
Polisi katika eneo la tukio

Bwana Mullen alisema mshukiwa anaaminika kuwa ni mtu hatari sana. Alisema shambulizi hilo linaangaliwa kama uhalifu wa chuki na kwamba idara ya FBI inasaidia katika uchunguzi.

Polisi walilazimika kuwaondoa majirani wanaozunguka eneo la kanisa baada ya kupokea kitisho cha bomu. Kitisho hicho baadae kiliondolewa.

Wakati huo huo Meya wa Charleston, Joseph Riley aliliita shambulizi hilo “tukio lisiloelezeka na lenye kutia machungu sana”.

XS
SM
MD
LG