Watu tisa akiwemo mtoto mchanga wamefariki baada ya boti yao kuzama wakati ikijaribu kuvuka bahari ya Mediterania katika hali ya hewa yenye dhoruba, na watu wengine 15 wanahofiwa kupotea, walinzi wa pwani ya Italia wamesema Alhamisi.
Walinzi wa pwani ya Italia wamesema walipokea ombi la ushirikiano kutoka kwa mamlaka ya utafutaji na uokoaji ya Malta (SAR) baada ya boti hiyo kuzama takriban kilomita 50 kusini mashariki mwa kisiwa cha Lampedusa siku ya Jumatano.
Walinzi wa pwani wamesema walipeleka boti yao ya doria katika eneo la tukio, ambapo iliwaokoa manusura 22 na kuwapata watu 9 wakiwa wameshakufa, akiwemo mtoto mchanga.
Operesheni za uokoaji zilikuwa na changamoto hasa kutokana na hali mbaya ya hewa kwenye bahari katika eneo hilo pamoja na mawimbi hadi mita 2.50, walinzi wa pwani walisema.
Forum