Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 11:30

Watu sita wauwawa Kenya


Kaunti ya Mandera, nchini Kenya

Takriban watu sita wameuawa leo Ijumaa baada ya watu waliokuwa na bunduki kushambulia mabasi mawili nchini Kenya karibu na mpaka wa Somalia.

Mkuu wa Polisi nchini Kenya amethibitisha kwamba maafisa wa polisi wamepata miili ya watu sita lakini akaongeza kuwa operesheni ya kuwasaka magaidi waliotekeleza mauaji hayo imeanza.

Raia wanne na maafisa wawili wa kulinda usalama ambao walikuwa wamejihami wanaaminika kuwa kati ya waliouawa.

Kulingana na gazeti la 'Daily Nation,' mashambulizi hayo yalitokea katika eneo la Elwak, kaunti ya Mandera, nchini Kenya.

Mashambulizi kama hayo katika eneo hilo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya yamekuwa yakitekelezwa na kundi la wanamgambo la Al-Shabaab, walio na makao yao katika nchi jirani ya Somalia.

XS
SM
MD
LG