Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 05:35

Watu saba wanusurika kifo katika bahari ya Pacific


Kikosi cha anga cha New Zealand kikiwaokoa manusura katika bahari ya Pacific, Jan. 28, 2018.
Kikosi cha anga cha New Zealand kikiwaokoa manusura katika bahari ya Pacific, Jan. 28, 2018.

Watu sita na mtoto mmoja waligundulika Jumapili wakiwa hawajitambui baada ya kuelea kwenye maji kwa zaidi ya wiki moja katika boti ndogo ya mbao kwenye bahari ya Pacific.

Kikosi cha anga cha New Zealand kiliwagundua watu hao wakati ikiwatafuta manusura wa boti ambayo ilizama wakati ikisafiri kati ya visiwa viwili katika taifa hilo dogo la Kiribati. Wafanyakazi wa kikosi cha anga walifanikiwa kudondosha vifaa ikiwemo maji na chakula kwa manusura hao.

“Kundi hilo lilionekana kupata faraja ya kuonekana na kupatiwa msaada” Josh Ashby kutoka kitengo kinachoratibu uokozi New Zealand, alisema.

Boti ya MV Buritaoi ilibeba abiria 50 na iliondoka kisiwa cha Nonouti Januari 18 kwa safari ya siku mbili ikielekea South Tarawa, maafisa wanasema. Shirika la habari la Reuters hata hivyo linasema kwamba wafanyakazi wa dharura wa New Zealand waliambia kuhusu kupotea kwa boti hiyo siku ya Ijumaa ikiwa ni siku nane baada ya boti hiyo kuondoka bandarini.

Kikosi cha anga cha New Zealand kinasema hakuna ishara ya kuwapata abiria 43 waliobaki.

XS
SM
MD
LG