Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 17, 2026 Local time: 18:56

Watu saba wafariki katika ajali ya moto ndani ya klabu ya muziki nchini Uhispania

Wazimamoto wakifanya kazi nje ya klabu ya muziki iliyoshika moto katika mji wa Murcia, kusini mashariki mwa Uhispania, Oktoba 1, 2023. Picha ya AP
Wazimamoto wakifanya kazi nje ya klabu ya muziki iliyoshika moto katika mji wa Murcia, kusini mashariki mwa Uhispania, Oktoba 1, 2023. Picha ya AP

Watu saba walifariki katika ajali ya moto ndani ya klabu ya muziki nchini Uhispania Jumapili asubuhi, huku juhudi za uokoaji zikiendelea.

Huduma za dharura zilisema kwenye mtandao wa X uliojulikana zamani kama Twitter, kwamba wafanyakazi wa zima moto waliendelea kufanya kazi kwenye eneo la tukio wakisema “kulikuwa uwezekano wa kuwapata waathirika zaidi.”

Waokoaji walisema walipewa taarifa mara ya kwanza nyakati za saa kumi na mbili asubuhi majira ya huko, kwamba moto ulikuwa umezuka katika klabu hiyo ya muziki yenye ghorofa mbili.

Baadaye walifanikiwa kuingia na kupata miili minne, na miili mingine miwili dakika 40 baadaye. Saa moja baadaye, ofisi ya mji wa Murcia ilithibitisha kuwa idadi ya vifo iliongezeka na kufikia saba.

Forum

XS
SM
MD
LG