Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 08:08

Watu 9 wauliwa katika matukio tofauti Afrika Kusini


Polisi waondoa maiti ya mtu aliyeuliwa kwenye baa Soweto, Afrika Kusini, Julai 10, 2022
Polisi waondoa maiti ya mtu aliyeuliwa kwenye baa Soweto, Afrika Kusini, Julai 10, 2022

Watu 9 wameuwawa mwishoni mwa wiki katika matukio matatu tofauti Afrika Kusini kulingana na polisi walotoa taarifa siku ya Jumapili.

Watu walokua na bunduki wamefetua risasi kundi la watu walokua wanacheza dadu kando ya barabara katika kitondoji cha mjini Johannesburg na kuwaua watu wane kati yao na kuwajeruhi wengine wawili.

Polisi wa Johannesburg wanasema shambulio hilo lilitokea jana usiku katika mtaa wa Lenasia, kitoingoji cha Thembelihle, wiki moja baada ya mashambulio mawili yaliyosababisha vifo vya watu 20 - 16 kwenye baa katika kitongoji cha Sweto, na wanne wengine kwenye baakatika mji wa Pietermaritzburg.

Mkuu wa polisi wa jimbo la Gauteng, Elias Mawela, ameleza sehemu ya mauwaji yaliyotokea jana ni ya 'kutisha' katika kitongoji cha kusini cha mji mkuu wa biashara wa afrika kusini.

Anasema watu hao walikua wamekaa wakicheza na kushambuliwa na watu wasiojulikana. Uchunguzi unafanyika amesema Mawela na wanawatafuta washambuliaji.

Katika tukio jingine mkuu wa polisi Mawela anasema huko huko Thembelihle, mtu mwenye umri wa miaka 36 alipatikana ameuliwa kwa risasi baada ya kuibiwa vitu vyake.

Wakati huo huo katika jimbo la Western Cape polisi wameanza uchunguzi kufuatia mauwaji ya watu watau Jumamosi usiku katika kitongoji cha Khayelitsha.

Karibu watu 20 000 huuliwa kila mwaka Afrika Kusini kati ya wakazi milioni 60.

XS
SM
MD
LG