Takriban watu wanane wakiwemo watoto waliuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika shambulio la ndege zisizo na rubani kwenye maonyesho katika eneo la Timbuktu kaskazini mwa Mali, waasi wa Tuareg walisema Jumanne.
Muungano wa waasi unaojulikana kama Permanent Strategic Framework for the Defence of the People of Azawad (CSP-DPA)
ulisema katika taarifa siku ya Jumatatu kwamba ndege isiyo na rubani ya Uturuki ilifanya mashambulizi kadhaa katika soko la ndani na makazi ya raia.
CSP-DPA ililaumu jeshi la Mali na washirika wake kwa shambulio hilo.
Wanajeshi wa Mali hawakujibu mara moja ombi la kutoa maoni yao juu ya tukio hilo.
Watuareg ni kabila ambalo wanaishi eneo la Sahara, ikiwa ni pamoja na sehemu za kaskazini mwa Mali, na wanapigania nchi huru.
Forum