Maafisa wa afya wa Misri wanasema watu 73 wameuwawa na mamia wengine kujeruhiwa jana jumatano katika ghasia kufuatia mechi ya mpira wa miguu katika mji wa kaskazini wa Port Said kwenye pwani ya Mediteranean.
Washabiki wa timu ya nyumbani ya al Masry walivamia uwanjani baada ya kupata ushindi ulio wa nadra sana dhidi ya timu ya timu kubwa ya Al Ahly.
Walirusha mawe, chupa na baruti kwa mashabiki kwa mashabiki wa wapinzani wao na wachezaji. Televisheni ilionyesha mashabiki wakikimbilia uwanjani na kuwafukuza wachezaji wa Al Ahly na kusababisha mapigano na mkanyagano. Picha hizo za televisheni pia zilionyesha moto uwanjani.