Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:26

Watu 70 wauwawa katika ghasia mwishoni mwa wiki Nigeria


Seneta wa serikali kuu Gyang Dantong mwakilishi wa jimbo la Plateau kaskazini na mbunge kiongozi wa walio wengi kwenye baraza la wawakilishi la bunge Gyang Fulani.

Wanasiasa wawili wa Nigeria wameuwawa kati kati ya Nigeria jana wakati wakishiriki mazishi ya watu wengi pamoja, ambao ni waathirika wa shambulizi lililotokea Jumamosi.

Maafisa wanasema seneta Gyang Dantong, na mbunge Gyang Fulani wa jimbo la Plateau Kaskazini ambae ni kiongozi wa wabunge walio wengi katika baraza la wawakilishi katika bunge la taifa ni miongoni mwa zaidi ya watu 20 waliouwawa wakati wa kushindikiza maiti Jumapili karibu na mji mkuu wa jimbo la Plateau, Jos. Wanasema mwanasiasa mmoja alinusurika shambulizi hilo.

Maafisa wanawalaumu wachungaji mifugo waislamu wa kabila la Fulani kwa shambulio hilo. Wabunge hao wawili walikuwa wa kabila la Birom. Viongozi wa kabila la Fulani walikana kuhusika na shambulizi la Jumapili.

Mapema Jumamosi magenge ya wenye silaha walishambulia vijiji viwili karibu na Jos, na kuuwa kiasi cha watu 50, ikiwa ni pamoja baadhi ya maafisa wa vikosi vya usalama vilivyojibu mashambulizi.

XS
SM
MD
LG