Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 21:26

Watu 7 wauwawa na 100 kutekwa Nigeria


Takriban watu saba waliuawa na 100 kutekwa Jumamosi usiku wakati watu wenye silaha waliposhambulia jamii ya vijijini katika jimbo la Katsina kaskazini magharibi mwa Nigeria, wakaazi na polisi wamesema Jumapili, likiwa shambulizi la karibuni kabisa kwa wakaazi kaskazini mwa nchi hiyo.

Magenge ya watu wenye silaha mara kwa mara yamekuwa yakivamia jamii za kaskazini-magharibi, na kuwateka nyara wakazi, wanafunzi na madereva wa magari ili kupata fedha.

Wakazi wamesema watu wenye silaha wakiwa kwenye pikipiki walifika katika kijiji cha Maidabino katika eneo la serikali ya mtaa wa Danmusa, Katsina, na kuanza kufyatua risasi mara kwa mara, na kuwafanya raia kukimbia.

Hassan Aliyu ameliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu kwamba shambulizi hilo liliwashangaza wakazi, wanawake na watoto ambao wamethibitishwa kutoweka.

Forum

XS
SM
MD
LG