Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 25, 2025 Local time: 04:30

Watu 7 wauawa katika shambulio la kujitoa mhanga Somalia


PICHA YA MAKTABA: Shambulizi la hoteli nchini Somalia
PICHA YA MAKTABA: Shambulizi la hoteli nchini Somalia

Takriban watu saba waliuawa Jumatano wakati magari mawili yaliyobeba vilipuzi, yalipolipulika nje ya kambi ya mafunzo ya kijeshi katika mji wa Bardhere, kusini mwa Somalia.

"Wanamgambo hao waliwalenga wanajeshi wa kikanda, kwa mabomu mawili ya kwenye gari. Wanajeshi saba waliuawa na takriban 18 kujeruhiwa,” Osman Nuh Haji, naibu gavana wa eneo la Gedo anayehusika na usalama, aliiambia VOA.

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika, mkuu wa wilaya ya Bardhere, Mohamed Wali Yusuf, alisema vikosi vya usalama vya mkoa, vilizuia mabomu ya kujitoa mhanga, ya kwenye gari, kufikia kambi inayotumika kwa ajili ya kuwaajiri watu.

"Tulikuwa tumepata vidokezo vya kiusalama kuhusu uwezekano wa mashambulizi, na hilo lilitusaidia kuzuia mashambulizi na kuzuia magari ya kujitoa muhanga kufikia eneo hilo," alisema Yusuf.

Wanamgambo wenye itikadi kali wa Al-Shabab walidai kuhusika na shambulizi hilo, wakisema "walilenga kambi hiyo kwa sababu maafisa wa Ethiopia na Somalia walikuwa wakikutana huko." Hata hivyo, mamlaka za eneo hilo zimekanusha madai hayo.

Mwezi Machi mwaka huu, shambulio kama hilo la bomu lililotegwa ndani ya gari, lililenga hoteli katika eneo hilo na kusababisha vifo vya wanajeshi kadhaa, na wengine 10 kujeruhiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG