Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:05

Mabaharia 7 wa Indonesia watekwa nyara


Serikali ya Indonesia imesema leo kuwa mabaharia wake 7 wametekwa nyara kwenye bahari ilioko kusini mwa Ufilipino ukiwa utekaji mpya kabisa kufanyika kwenye maji kati ya nchi zote mbili.

Maafisa wa Indonesia wamesema kuwa mabaharia 13 walikuwa kwenye boti iliokuwa imebeba makaa kwenye bahari ya Sulu hapo jana Jumatatu wakati ilipotekwa nyara na watu wenye silaha.

Waziri Mkuu wa Indonesia, Rento Marsudi, amesema watafanya lote wawezalo kuhakikisha mateka hao saba wamechiliwa.

Maafisa kutoka Jakarta hawajadhibitisha iwapo kuna fedha zinazoitishwa na watekaji nyara au hata kama watu hao ni kutoka kundi la wapiganaji lenye makao yake kusini mwa Ufilipino la Abu Sayyaf.

Kundi hilo la Abu Sayyaf lilianza likiwa la uasi likiitisha serikali tofauti ya kiislamu na inasemekana lilipata misaada ya kifedha kutoka kwa kundi la al Qaida miaka ya 90.

XS
SM
MD
LG