Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:16

Watu 7 wafariki kwa kukanyagwa kwenye kandanda Kenya


Mashabiki wa Gor Mahia wakati wa mchuano na timu ya AFC Leopard.
Mashabiki wa Gor Mahia wakati wa mchuano na timu ya AFC Leopard.

Mashabiki wasiokua na tiketi walijaribu kutumia nguvu kuingia kwenye uwanja wa michezo wa Nayo mjini Nairobi, siku ya Jumamosi na kusababisha msukumano mkubwa ulopelekea watu saba kufariki kutokana na kukanyagwa na wengine 12 kujeruhiwa.

Mashirika ya habari yanaripoti kwamba, watu ambao hawakuweza kununuwa tiketi zao walipofika uwanjani kutizama mchunao kati ya timu za AFC Leopard na Gor Mahia, walijaribu kuingia kwa nguvu.

Mchuano ulisimamishwa kwa muda hadi walojeruhiwa kuhudumiwa kabla ya mchezo kuendelea, ambapo Gor Mahia ilipata ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya AFC.

Msemaji wa shirika la Msalaba Mwekundu anasema, watu sita walifariki uwanjani na mmoja alifariki hospitali kutokana na majeraha aliyoyapata. Mashahidi wanalilaumu shirikisho la kandanda la Kenya kwa maandalizi mbaya yaliopelekea mashabiki wengi kutoweza kuingia uwanjani baada ya kufungwa milango mchezo ulipoanza.

Shirikisho la Kandanda la Kimataifa FIFA, limeshapendekeza kwa shirikisho la kandanda la Kenya siku za nyuma kuuza tiketi siku moja kabla ya mchuano ili kuepukana na matatizo kama hayo.

XS
SM
MD
LG