Watu 64 wamefariki katika ajali ya meli kwenye ufukwe wa kaskazini-mashariki mwa Madagascar na msako unaendelea kuwatafuta abiria 24 ambao hawajulikani walipo shirika la usafiri wa majini lilisema Jumatano.
Watu 50 walionusurika walipatikana shirika la Maritime and River Port lilisema. Meli hiyo ni meli ya mizigo ambayo haikuidhinishwa kusafirisha watu na ilijaza kupita kiasi na maji yalijaa kwenye injini alisema Mamy Randrianavony mkurugenzi wa operesheni za bahari kwenye shirika la Maritime and River Port (APMF).
Meli ilizama Jumatatu usiku ikiwa na watu 138 kulingana na maelezo ya APMF.