Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 07:12

Watu 62 wamefariki Sudan kutokana na mvua pamoja na mafuriko


Mvua kubwa pamoja na mafuriko vimesababisha vifo 62 na nyumba takribani 37,000 zimeharibiwa huko Sudan
Mvua kubwa pamoja na mafuriko vimesababisha vifo 62 na nyumba takribani 37,000 zimeharibiwa huko Sudan

Mvua kubwa za msimu zinazoendelea nchini humo zimeathiri takribani watu laki mbili. Umoja wa mataifa umesema zaidi ya nyumba 37,000 ziliharibiwa ikinukuu idadi kutoka ofisa wa serikali anayehusika kutoa majibu katika matukio ya majanga ya kiasili

Shirika rasmi la habari la Sudan-SUNA limeripoti kuwa mvua kubwa pamoja na mafuriko yameuwa watu 62 nchini humo na kuwajeruhi watu 98 wengine.

Sudan imekumbwa na mvua kubwa za msimu tangu mwanzoni mwa mwezi Julai ambapo zimeathiri takribani watu laki mbili katika majimbo yapatayo 15 kote nchini humo ikiwemo mji mkuu Khartoum. Eneo lililoathiriwa vibaya ni jimbo la West Nile lililopo kusini mwa nchi hiyo.

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulisema watu 54 walikufa kutokana na mvua kubwa. UN ilisema zaidi ya nyumba 37,000 ziliharibiwa ikinukuu idadi kutoka ofisa wa serikali anayehusika kutoa majibu kufuatia matukio yanayosababishwa na majanga ya kiasili. UN ilisema kwamba wafanyakazi wa kutoa msaada wa dharura wana wasi wasi wa kutokea mafuriko zaidi ikiongeza kuwa msimu wa mvua ulitarajiwa kuendelea hadi Oktoba mwaka huu.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika kuratibu masuala ya kibinadamu ilisema dola milioni 15 za ziada zilihitajika kutoka kwa wafadhili katika kukabiliana na hali ya dharura iliyojitokeza ikiongezwa kwenye mfuko wa dola bilioni 1.1 zilizotakiwa kwa ajili ya kukabiliana na shughuli nzima za dharura nchini Sudan.

XS
SM
MD
LG