Mfanyakazi wa hospitali ya karibu ya Al-Nao, akiomba kutotajwa, amesema idadi ya waliofariki ni kubwa katika tukio ambalo inadaiwa limefanywa na wanamgambo wa kikosi cha akiba (RSF).
Toka Aprili 2023, wanamgambo wa RSF wamekuwa kwenye vita na jeshi la Sudan, katika mzozo mbaya ambao umeua maelfu ya watu na kuwafanya watu zaidi ya milioni 12 kukosa makazi.
Mhudumu wa kujitolea katika Hospitali ya Al-Nao, ameiambia AFP kwamba walikuwa wakihitaji sana sanda, wachangiaji damu na machela ili kuwasafirisha waliojeruhiwa.
Hospitali hiyo ni mojawapo ya vituo vya mwisho vya matibabu vinavyofanya kazi katika eneo hilo, na imekuwa ikishambuliwa mara kwa mara.
Forum