Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 04, 2023 Local time: 04:34

Watu 41 wafariki kwenye ajali ya basi Mali


Picha ya ajali tofauti kutoka kwenye maktaba

Wizara ya uchukuzi ya Mali imesema Jumanne kwamba watu 41 wamekufa baada ya lori la mizigo lililokuwa pia limebeba wafanyakazi kugongana na basi walilokuwa wakisafiria.

Chombo cha habari cha serikali cha ORTM kimesema kwamba gurudumu la lori hilo lilipasuka na kusababisha dereva wake kushindwa kulidhibiti na ndipo liliserereka upande wa basi na kugongana ana kwa ana.

Shirika la habari la Reuters linasema kuwa ajali hiyo ilitokea kiasi cha kilomita 20 kutoka mji wa Segou ambako sehemu ya mbele ya basi hiyo iliharibiwa kabisa kulingana na picha na video zilzowekwa mtandaoni.

Msemaji wa wizara ya uchukuzi Mohamedoune Ould Mamouni ameongeza kusema kuwa watu 33 walijerujiwa wakati wa ajali hiyo. Kulingana na takwimu kutoka shirika la afya duniani WHO, Afrika ndiyo yenye bara bara hatari zaidi ulimwenguni ambapo vifo 26 kutokana na ajali kutokea kwa kila idadi ya watu 100,000.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG