Mvua kubwa imesababisha mafuriko ambayo yameua watu 40 kaskazini mwa India.
Watu kadhaa hawajulikani walipo.
Taarifa ya serikali imesema kwamba karibu watu 36 waethibitishwa kufariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika eneo la Himalaya, jimbo la Himachal Pradesh, katika muda wa siku tatu.
Watu wanne wamefariki katika jimbo la Uttarakhand, na 13 wengine hawajulikani walipo baada ya mito kuvunja kingo na maji kuingia kwenye makaazi ya wat una kusababisha uharibifu mkubwa.