Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 06:59

Watu 140 wafariki baada ya lori la mafuta kulipuka Pakistan


Afisa wa kulinda usalama anasimama katika eneo ambapo watu wapatao 140 walipoteza maisha yao baada ya lori la mafuta kulipuka nchini Pakistan tarehe 25, Juni, 2017.
Afisa wa kulinda usalama anasimama katika eneo ambapo watu wapatao 140 walipoteza maisha yao baada ya lori la mafuta kulipuka nchini Pakistan tarehe 25, Juni, 2017.

Maafisa wa serikali ya Pakistan walisema Jumapili kwamba lori lililokuwa limebeba mafuta lililipuka moto  na kuwaua watu wasiopungua 140, ambao walikuwa wameenda pahali lori hilo lilikuwa limevingirika, ili kuchota mafuta yaliyokuwa yakivuja.

Mamlaka zilisema kuwa takriban watu 80 walikuwa wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo na wengi wao walikuwa katika hali mahututi.

Lori hilo lilikuwa kikiendeshwa kwenye barabara kuu kutoka mji wa bandari wa Karachi, kuelekea Lahore, ulio mji mkuu wa jimbo la Punjab, wakati dereva alishindwa kulidhibiti na likavingirika.

Mkuu wa polisi katika eneo hilo, Raja Riffat, alisema kwamba baada ya lori hilo kuvingirika, wakazi wanaoishi karibu na eneo la ajali hiyo walikimbia kuelekea lori hilo lilipokuwa huku wakibeba ndoo na vyombo vingine vya kuchotea mafuta.

Aidha, kundi kubwa la watu waliobebwa na pikipiki walijiunga nao ili kuchota mafuta yaliyokuwa yakivuja.

Mkasa huo ulitokea mkesha wa sikukuu ya Idd Al Fitr, kuadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi wa Ramadan.

Kwa kawaida, barabara za eneo hilo huwa zimejaa watu wakati kama huu, huku watu wakisafiri kwenda kuungana na familia zao kusherehekea sikukuu ya Eid.

Chanzo cha mlipuko huo, hakikujulikana mara moja.

XS
SM
MD
LG