Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 19:01

Watu 35 watoweka katika mafuriko mabaya kusini mwa Ukraine


Picha ya mafuriko katika kitongoji cha mkoa wa Kherson, Juni 8, 2023.
Picha ya mafuriko katika kitongoji cha mkoa wa Kherson, Juni 8, 2023.

Watu 35 wakiwemo watoto saba, wametoweka Jumapili kusini mwa Ukraine kufuatia mafuriko mabaya yaliyotajwa na waendesha mashtaka kama “janga baya la mazingira tangu janga la nyuklia la Chernobyl.”

Bwawa la Kakhovka linalodhibitiwa na Russia kwenye uwanja wa mapigano katika mkoa wa Kherson liliharibiwa tarehe 6 Juni, na kulazimisha maelfu ya watu kukimbia na kuzua hofu ya mzozo wa kibinadamu na janga la mazingira.

Ukraine iliishtumu Russia kulipua bwawa hilo kwenye mto Dnipro, huku Moscow ikisema kwamba Kyiv ndiyo ilishambulia jengo hilo.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine Igor Klymenko amesema miji 77 na vijiji vimefunikwa na maji katika mikoa ya kusini ya Kherson na Mykolaiv.

Kutokana na mafuriko hayo, watu watano walifariki katika mkoa wa Kherson na mtu mmoja alifariki katika mkoa wa Mykolaiv.

Jumla ya watu 3,700 walihamishwa kutoka kwenye makazi yao katika mikoa hiyo miwili, waziri huyo wa mambo ya ndani alisema katika taarifa.

Forum

XS
SM
MD
LG