Watu wasiopungua 32 waliuawa na wengine 63 wamejeruhiwa baada ya wanamgambo wa al-Shabab kushambulia eneo la mbele la ufukwe ulilojaa watu mjini Mogadishu nchini Somalia, Ijumaa usiku, kulingana na msemaji wa polisi wa Somalia, Meja Abdifatah Aden Hassan.
Shambulio hilo lilianza majira ya saa nne usiku kwa saa za huko kwa mlipuko wa bomu la kujitoa muhanga katika ufukwe uliojaa watu, wakati watu hao walipokuwa wakifurahia wikiendi. Kanda za video zilizochapishwa na vyombo vya habari zilionyesha watu wengi wakiwa wamelala ufukweni, wengine wakiwa wamekufa na wengine kujeruhiwa vibaya.
Baada ya mlipuko wa kwanza kutokea, washambuliaji watatu wenye silaha wa al-Shabaab walivamia jengo la chakula na burudani katika ufukwe huo. Licha ya raia hao kuuawa, washambuliaji wote watatu walipigwa risasi na kuuawa na vikosi vya usalama, polisi wamesema. Mwanamgambo wa nne alijilipua mwenyewe, ripoti hiyo iliongeza.
Forum