Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 23:22

Watu 22 wafariki katika ajali ya helikopta mbili za jeshi la Uganda mashariki mwa DRC


Gari la doria la jeshi la Uganda laonekana wakati wa operesheni ya kuwasaka waasi wa ADF karibu na Semuliki, Disemba 10, 2021. Picha ya AFP

Watu 22 wamefariki katika ajali ya helikopta mbili za jeshi la Uganda zilizoanguka mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, msemaji wa jeshi la Congo ambaye hakutaka jina lake litajwe ameliambia shirika la habari la Reuters Jumatano.

Uganda ilipeleka wanajeshi wake nchini DRC mwezi Disemba mwaka jana kuisaidia nchi hiyo kupambana na waasi wa kundi la Alliance Democratic Forces (ADF).

Msemaji huyo wa jeshi la DRC ameiambia Reuters kwamba “ jeshi la Uganda halijatueleza mazingira ya ajali hiyo,” akiongeza kuwa imehusisha helikopta mbili.

Amesema ni watu 22 walifariki bila pia kupata maelezo zaidi.

Msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye amethibitisha kwamba helikopta ya kwanza ilifanya ajali Jumatatu katika kijiji cha Boga jimbo la Ituri, huku helikopta ya pili ikianguka katika eneo la mpaka la Kabarole kati ya nchi hizo mbili.

Afisa mwengine amesema wanajeshi watatu wa Congo walifariki katika ajali ya kwanza, lakini hakikufafanua ikiwa walikuwa ndani ya helikopta au aridhini.

ADF ilianza kama kundi la uasi nchini Uganda lakini imekuwa na ngome zake nchini Congo tangu mwishoni mwa mwaka wa 1990.

Uganda ililishtumu kundi hilo kwa kuhusika katika mashambulizi matatu ya bomu mjini Kampala tarehe 16 Novemba mwaka jana, ambayo yaliua watu 7 wakiwemo washambuliaji wa kujitoa muhanga.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG