Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 04:19

Watu 18 wauwawa katika jimbo la  Ituri mashariki mwa DRC


Watu waliokimbia vita wameketi katika kambi huko Komanda, mkoa wa Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Agosti 30, 2023.AFP
Watu waliokimbia vita wameketi katika kambi huko Komanda, mkoa wa Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Agosti 30, 2023.AFP

Watu wenye silaha walishambulia kijiji kimoja katika jimbo la Ituri mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo siku ya Alhamisi, na kuuwa takriban watu 18 na kujeruhi wengine 12, afisa wa eneo hilo alisema.

Eneo hilo linakumbwa na maelfu ya makundi mkchanganyiko yenye silaha na ghasia zimewalazimisha mamilioni kukimbia makazi yao.

Kanali Jean Siro Simba Bunga, msimamizi wa eneo la Irumu ambako shambulio hilo lilitokea, alisema washambuliaji walichoma miili mitatu lakini wengine 15 watazikwa.

Tunasikitishwa na hali hii alisema, akiwalaumu wanamgambo wa eneo hilo kwa vifo visivyo vya lazima.

Manusura Alain Kalito anasema watoto walikuwa ni miongoni mwa waathirika na baba yake alijeruhiwa vibaya.

Forum

XS
SM
MD
LG