Mamia zaidi ya watu wamejeruhiwa kwa mujibu wa maafisa, na baadhi ya watu walikwama chini ya vifusi.
Vifo vingi vimetokea nchini Ecuador.
Idara ya huduma za hali ya hewa ya Marekani haikutoa tahadhari ya Tsunami kabla ya kutokea kwa tetemeko hilo.
Shirika la habari la Associated Press, limeripoti kwamba nchini Ecuador, nyumba nyingi ambazo zimeanguka zimefanana na ni makazi ya watu masikini, zilikuwaz nyumba za zamani na hazikukidhi viwango vya ujenzi katika nchi hiyo iliyo na hatari ya kukumbwa na tetemeko la ardhi.