Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 03:50

Watu 14 wamekufa katika mapambano ya kudhibiti makao makuu ya polisi Khartoum


Magari ya kivita ya jeshi la Sudan yakiendeshwa barabarani mjini Khartoum, Juni 26, 2023. Picha na AFP
Magari ya kivita ya jeshi la Sudan yakiendeshwa barabarani mjini Khartoum, Juni 26, 2023. Picha na AFP

Jeshi la Sudan limekabiliwa na mashambulizi kutoka sehemu mbali mbali siku ya Jumatatu baada ya kupoteza udhibiti wa makao makuu ya polisi kwa wanamgambo wakati wa mapigano Jumapili katika mji mkuu wa Khartoum, yaliyosababisha vifo vya takriban watu 14

Kikosi cha dharura cha (RSF), ambacho tangu katikati ya mwezi Aprili kimekuwa kikipigana na jeshi la Sudan, kilitangaza Jumapili usiku kwamba "kimepata ushindi katika kupigania makao makuu ya polisi".

"Makao makuu yako chini ya udhibiti kamili... na tumeteka idadi kubwa ya magari, silaha na silaha," RSF ilisema katika taarifa yake, na tumechukua udhibiti wa magari ya kubebea mizigo, magari ya kivita na vifaru.

Wakati huo huo kikosi cha (RSF) kimesema kimeteka makao makuu ya kitengo cha polisi kilichokuwa na silaha nzito Jumapili wakati kikitafuta ushindi katika vita vyake na jeshi wakati wa mapigano makali katika mji mkuu Khartoum.

RSF ilisema katika taarifa kwamba imechukua pia udhibiti kamili wa kambi ya Polisi wa Akiba iliyopo kusini mwa Khartoum, na kubandika picha za wapiganaji wake wakiwa ndani ya kituo hicho, baadhi yao wakiondoa masanduku yenye risasi kutoka kwenye ghala.

Reuters haikuweza mara moja kuthibitisha picha au taarifa hizo za RSF. Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusiana na taaifa hizo kutoka jeshi la Sudan au polisi.

Tangu Jumamosi jioni, mapigano yaliongezeka katika miji mwili inayoungana na mji mkuu wa Khartoum, wa Bahri na Omdurman - wakati mzozo huo wa kati ya jeshi na RSF ukiingia wiki yake ya 11.

Mashahidi pia waliripoti ongezeko kubwa la ghasia katika siku za hivi karibuni huko Nyala, jiji kubwa zaidi uliopo katika jimbo la magharibi la Darfur. Umoja wa Mataifa ulitoa tahadhari Jumamosi kuhusu mashambulio ya kikabila na mauaji ya watu kutoka jamii ya Masalit iliyoko El Geneina huko Darfur Magharibi.

Khartoum na El Geneina ni maeneo yaliyoathiriwa zaidi na vita, ingawa wiki iliyopita mivutano na mapigano yaliongezeka katika maeneo mengine ya Darfur na Kordofan upande wa kusini.

Chanzo cha bahari hii ni mashirika la habari la Reuters na AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG