Watu wenye bunduki, wakitumia usafiri wa pikipiki, wameshambulia vijiji vine katika sehemu ya Kanam, na kuua watu kadhaa wakiwemo watoto na vijana.
Polisi wamethibitisha kutokea mauaji hayo, lakini hawajatoa maelezo zaidi.
Washambuliaji waliiba mifugo na kuchoma moto nyumba kadhaa.
Mamia ya watu wameachwa bila makao na baadhi ya hawajulikani walipo.
Nigeria inakabiliwa na matukio mengi ya makundi yenye silaha kushambulia vijiji, kuua watu na kuteka nyara.