Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:44

Watu 130 wauawa na wanamgambo wa kiislamu nchini Mali


Kanali Assimi Goita , kiongozi wa serikali ya mpito ya kijeshi akizungumza na waandishi wa habari mjini Bamako, Agosti 19, 2020. Picha ya AFP
Kanali Assimi Goita , kiongozi wa serikali ya mpito ya kijeshi akizungumza na waandishi wa habari mjini Bamako, Agosti 19, 2020. Picha ya AFP

Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu waliua zaidi ya raia 130 mwishoni mwa juma katika miji jirani ya katikati mwa Mali, ikiwa ni mauaji ya hivi karibuni katika eneo hilo la Sahel lenye mzozo.

Maafisa wa eneo hilo wameripoti matukio ya mauaji ya kiholela yaliyofanywa na watu wenye silaha huko Diallassagou na miji miwili jirani katika eneo la Bankass, eneo la Sahel ambalo limekuwa lenye machafuko kwa muda mrefu.

"Walichoma pia vibanda, nyumba na kuiba ng'ombe," amesema afisa wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu za kiusalama.

Yeye na afisa mwingine ambao wote wawili walikimbia kijiji chao, wamesema hesabu ya watu waliouawa ilikuwa ikiendelea Jumatatu.

Nouhoum Togo, afisa wa mji wa Bankass, mji mkubwa katika eneo hilo, amesema idadi ya waliouawa ni kubwa kuliko ile ya watu 132 iliyotangazwa na serikali, ambayo iliwashtumu wanamgambo wa kiislamu washirika wa Al-Qaeda kwa mauaji hayo.

XS
SM
MD
LG