Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:52

Watu 13 wafariki katika mapigano makali Syria

Baadhi ya watu wakiandamana Syria
Baadhi ya watu wakiandamana Syria

Wanaharakati wanasema mashahidi wameripoti kusikia milio ya milipuko na risasi nzito wakati vikosi vya Serikali vinapambana kaskazini magharibi mwa mji wa Binnish kwenye jimbo la Idlib.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamesema mapigano baina ya vikosi vya usalama vya serikali na watu wenye silaha wanaodhaniwa kuwa wamejitenga na jeshi yamesababisha vifo vya watu 13 kote Syria.

Kundi hilo la ufuatiliaji wa haki za binadamu lenye makao yake mjini London limesema mapigano karibu na mpaka wa uturuki leo yaliuwa watu watano.

Wanaharakati wanasema mashahidi wameripoti kusikia milio ya milipuko na risasi nzito wakati vikosi vya Serikali vinapambana kaskazini magharibi mwa mji wa Binnish kwenye jimbo la Idlib.

Wanaharakati wamesema mapigano mengine baina ya vikosi vya serikali na wanaume wanaodhaniwa kuwa walijenga na jeshi yalifanyika katika jimbo la Daraa kituo cha maandamano ya kuipinga Serikali.

Wanasema takriban watu nane walikufa wakiwemo wanajeshi sita.

XS
SM
MD
LG