Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 22, 2025 Local time: 13:10

Watu 1,100 wamekamatwa Ethiopia tangu ilipotangazwa hali ya dharura


Maandamano nchini Ethiopia
Maandamano nchini Ethiopia

Vyombo vya habari huko Ethiopia vimeripoti Jumamosi kwamba zaidi ya watu 1,100 wamekamatwa tangu nchi hiyo ilipotangaza hali ya dharura kufuatia kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wake mwezi uliopita. Hatua isiyotegemewa ya kujiuzulu Hailemariam Desalegn imekuja baada ya zaidi ya miaka miwili ya maandamano ya kuipinga serikali na kuongezeka mgawanyiko katika chama tawala nchini humo.

Waziri Mkuu mteule wa Ethiopia, Abiy Ahmed
Waziri Mkuu mteule wa Ethiopia, Abiy Ahmed

Chama cha Ethiopian People’s Revolutionary Democratic Front-EPRDF kwa mara ya kwanza kimemteuwa kiongozi wake kutoka kabila la Oromo, Abiy Ahmed. Kiongozi huyo anatarajiwa kuapishwa kama Waziri Mkuu mpya mwanzoni mwa wiki ijayo. Radio Fana yenye uhusiano na redio ya taifa ilisema watu 1,107 wamekamatwa kwa kukiuka amri ya dharura, ambayo inasitisha kwa muda katiba na kuwaruhusu polisi kuwashikilia watu bila kuwafungulia mashtaka.

Fana iliripoti ikimnukuu Tadesse Hordofa, mwenyekiti wa bodi inayoangalia amri hiyo kwamba watu hao walikamatwa kwa kuwauwa raia wasio na hatia na vikosi vya usalama, kuchoma moto nyumba na taasisi za kifedha, kuharibu majengo ya serikali na taasisi za umma pamoja na kufunga barabara.

XS
SM
MD
LG