Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 22:30

Watu 11 wameuwawa katika kambi ya kijeshi Cape Verde


Kikosi cha NRF-Nato Response Force kikifanya uangalizi wakati wa mazoezi ya ndege za NATO huko Sao Vicente, Cape Verde.
Kikosi cha NRF-Nato Response Force kikifanya uangalizi wakati wa mazoezi ya ndege za NATO huko Sao Vicente, Cape Verde.

Watu 11 wakiwemo wanajeshi 8 wameuwawa katika kambi ya kijeshi nchini Cape Verde.

Maafisa wa taifa hilo la Afrika Magharibi wanasema mwanajeshi mmoja mwenye malalamiko ambaye mpaka sasa hajulikani alipo, ndiye anayedhaniwa kufanya mauaji hayo ya wanajeshi na raia watatu ikijumuisha raia wawili wa Hispania.

Taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa serikali imesema, masuala binafsi ndiyo yaliyochochea kufanyika kwa shambulizi hilo, na kusema halikuwa jaribio la mapinduzi ama mzozo wa dawa za kulevya.

Vikosi vya usalama vimewekwa katika hali ya tahadhari katika uwanja wa ndege wa Praira, mji mkuu wa Cape Verde na bandari za kisiwa hicho baada ya miili hiyo kugundulika mnamo mida ya saa sita mchana jana Jumanne.

XS
SM
MD
LG