Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:14

Watu 11 wafariki katika ajali ya ndege nchini Cameroon


Ramani ya Cameroon
Ramani ya Cameroon

Ndege iliyokuwa inabeba watu 11 imefanya ajali Jumatano katika msitu katikati mwa Cameroon, wizara ya usafiri imesema.

Wafanyakazi wa usafiri wa anga walipoteza mawasiliano na ndege hiyo ambayo ilionekana baadaye ndani ya msitu karibu na kijiji cha Nanga Eboko, umbali wa kilomita 150 kaskazini mashariki mwa mji mkuu Yaounde, wizara ya usafiri imesema katika taarifa.

Afisa wa wizara hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema, ndege hiyo ilianguka na waokoaji walikuwa wanajaribu kuona ikiwa inawezekana kuokoa mtu yeyote.

Ndege hiyo ilikuwa imekodishwa na kampuni ya kibinafsi ya Cameroon ya usafirishaji wa mafuta (COTCO), inayosimamia bomba la hydrocarbon ambalo linapita kati ya Cameroon na nchi jirani ya Chad, vyanzo rasmi vimeiambia AFP.

Ndege hiyo ilikuwa inasafiri kutoka uwanja wa ndege wa Yaounde-Nsimalen kuelekea Belabo, mashariki mwa nchi, wizara ya usafiri imesema katika taarifa.

XS
SM
MD
LG