Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 10:55

Watu 100 wauwa Sudan Kusini


 Msuluhishi wa Sudan Kusini Pagan Amum katika mkutano na waandishi wa habari .
Msuluhishi wa Sudan Kusini Pagan Amum katika mkutano na waandishi wa habari .

Watu wapatao 100 wameuwawa na wengine mamia kadhaa wajeruhiwa katika mapigano ya Sudan Kusini.

Maafisa wa Sudan Kusini wanasema watu wapatao 100 wameuwawa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika mapigano mapya ya kikabila. Gavana wa jimbo la Jong’lei Kuol Manyang alielezea idadi ya waliojeruhiwa katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu. Kamishna wa kitongoji cha Akobo Pal Mai alisema mapigano yalianza mwishoni na kuendelea kwa siku nzima. Shambulio la mwisho lilitokea kuamkia siku iliyopangwa kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano na kupunguza mvutano katika jimbo hilo la Jong’lei.

XS
SM
MD
LG