Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, watu waliokuwa na silaha wameshambulia kijiji cha Masala karibu na mji wa Beni ambao uko katika jimbo la Kivu Kaskazini, usiku wa kuamkia leo, kiongozi wa kijeshi Charles Euta Omeonga, ameiambia Reuters kwa njia ya simu.
Kiongozi wa asasi za kiraia Justin Kavalami amesema kuwa shambulizi hilo limefanywa na vikosi vya kundi la Allied Democratic Forces, ADF, ambalo maafisa wa kieneo wanadai kuwa lilifanya shambulizi kwenye kijiji tofauti mapema wiki hii na kuuwa takriban watu 16.
Kavalami ameongeza kusema kuwa zaidi ya watu 13 wameuwawa kwenye shambulizi la Masala. Kundi la ADF lilianzia Uganda, wakati makao yake makuu yakiwa Mashariki mwa Congo, huku likiwa tiifu kwa kundi la kigaidi la Islamic State. Juhudi za Reuters za kufikia kundi hilo hazikufua dafu wakati wa kuchapishwa kwa ripoti hii.
Forum